Mradi wa umeme Rusumo wakamilika kwa asilimia sitini

0
174

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) imeeleza kuridhishwa na ujenzi unaoendelea wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Rusumo utakaokua na uwezo wa kuzalisha megawati themanini za umeme.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt Alexandra Kiyaruzi amesema kuwa, ujenzi umekamilika kwa asilimia sitini hadi sasa na unatarajiwa kukamilika mwezi februari mwaka 2021.

Umeme utakaozalishwa utatumika katika nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi ambapo Tanzania itapata megawati 27 za umeme utakaotumika mkoani Kagera.