Mradi wa maji wa Nangomba wazinduliwa

0
95

Mwenge wa Uhuru umeridhia kuzindua mradi wa maji wa Nangomba katika kijiji cha Nangomba wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amesema katika miradi ya maji mitano aliyokagua katika mkoa wa Mtwara, mradi huo wa maji wa Nangomba angalau umefanya vizuri.

Luteni Mwambashi amesema miradi mingi ya maji mkoani Mtwara utekelezaji wake hauridhishi, na hivyo kuleta adha kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa Wananchi.

Amewataka wataalam wa maji wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kufanya kazi kwa uzalendo, ili miradi hiyo itoe huduma bora kwa Wananchi.

Mradi huo wa maji wa Nangomba utanufaisha zaidi ya Wakazi mia nne wa vijiji vya Nangomba na Mji Mwema ambao kwa muda mrefu walikuwa na kero ya maji.

Chanzo cha maji cha mradi huo ni kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha lita mia sita kwa saa, na ulianza kutekelezwa mwezi Mei mwaka 2020 na kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Mwenge wa Uhuru umeridhia kuzindua mradi wa maji wa Nangomba katika kijiji cha Nangomba wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi amesema katika miradi mitano ya maji aliyokagua mkoani Mtwara, mradi huo wa maji wa Nangomba angalau umefanya vizuri.

Luteni Mwambashi amesema miradi mingi ya maji mkoani Mtwara utekelezaji wake hauridhishi, na hivyo kuleta adha kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Amewataka wataalam wa maji wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kufanya kazi kwa uzalendo, ili miradi hiyo itoe huduma bora.

Mradi huo wa maji wa Nangomba utanufaisha zaidi ya wakazi 400 wa vijiji vya Nangomba na Mji Mwema ambao kwa muda mrefu walikuwa na kero ya maji.

Chanzo cha maji cha mradi huo ni kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha lita mia sita kwa saa, na ulianza kutekelezwa mwezi Mei mwaka 2020 na kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Mradi wa maji wa Nangomba umekamilika kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200, fedha ambazo ni kutoka Serikali kuu kwa kushirikisha nguvu za Wananchi.

Mradi wa maji wa Nangomba umekamilika kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200, fedha ambazo ni kutoka Serikali kuu kwa kushirikisha nguvu za Wananchi.