MPOKASYE: MKAPA KIONGOZI IMARA

0
188

Edwin Mpokasye, Mkurugenzi wa Kituo cha Redio Fadhila, Masasi mkoani Mtwara amesema anamfahamu Marehemu Rais Benjamin Mkapa kama kiongozi imara aliyeweza kuiongoza Tanzania kwa weledi.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mpokasye amesema kuwa Rais Mkapa alikumbana na changamoto nyingi kama vile machafuko ya Mwembechai, lakini aliweza kuyatatua yote kwa majadiliano.

Akizungumzia sera ya ubinafsishaji iliyotekelezwa na kiongozi huyo, Mpokasye amesema lilikuwa ni jambo muhimu kufanywa kwa wakati ule, na kwamba wote waliopinga, walifanya hivyo kwa sababu hawakuwa na uelewa wa kwanini ubinafsishaji ulitakiwa kufanyika.

Amesema njia bora ya kumuenzi kiongozi huyo ni kusoma historia yake, mathali kitabu alichoandika (My Life My Purpose) ili kujua adhma ya mambo mengi aliyoyatenda.

Rais Benjamin Mkapa ndiye aliyeizindua Redio Fadhila (redio ya jamii) mwaka 2015.