Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, bunge, kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewataka watendaji wanaohusika na afua za lishe nchini kusimamia vema taratibu za upatikanaji na ulaji wa lishe bora ili kujenga taifa imara na lenye nguvu.
Waziri Jenista ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati alipokua akitoa taarifa ya mpango jumuishi wa kwanza wa lishe ulioanza rasmi nchini kwenye mwaka wa fedha 2014/ 2015.
Amesema swala la lishe ni swala linalotakiwa kupewa kipaumbele kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa lengo likiwa ni kutoa makuzi bora ili kuepuka udumavu.
Aidha amesema mpango jumuishi wa kwanza wa lishe umefanikiwa Kwa asilimia 80 ya malengo waliojiwekea na viashiria kuleta matokeo chanya.
Mkutano wa Saba wa mpango jumuishi wa pili wa lishe Kitaifa utafanyika Novemba 18 jijini Tanga na unatarajia kufunguliwa na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa na baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu.