Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amezindua rasmi Hati Fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 50 akisema ni ya kihistoria.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dkt. Mpango amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga kwa asilimia 100.
Aidha, Dkt. Mpango ameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Masoko, Mitaji na Dhamana kwa kupitisha hati fungani hiyo muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya taifa.
Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Rais ameiagiza Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kuweka utaratibu wa mifumo ya tahadhari ili kufuatilia vihatarishi vinavyoweza kujitokeza kwenye utekelezaji wa hati fungani hiyo.
Pia amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ikiwemo sekta binafsi kushiriki katika ununuzi wa hati fungani hiyo ili waweze kushiriki kwa vitendo kuunga mkono nia ya serikali ya kuwatetea wananchi maendeleo.