Mpango afungua warsha ya utekelezaji wa Haki Jinai

0
154

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amefungua Warsha ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai .

Akifungua Warsha hiyo jijini Dodoma Makamu wa Rais amesema azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwepo kwa mfumo imara, wenye kuzingatia haki na misingi ya utawala bora katika kuwahudumia wananchi.

Ameongeza kwamba nia ya dhati ya Rais ni kuleta mapinduzi ya kifikra na mabadiliko ya kimfumo katika utendaji wa taasisi za Haki Jinai hapa nchini.

Makamu wa Rais amewataka Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kutekeleza ipasavyo mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kwa kuwa Wananchi wameonesha hitaji la mabadiliko katika utendaji wa taasisi za haki jinai ili kuongeza uwezo na kuhakikisha haki inatendeka.

Amewasihi kufahamu kwa kina msingi wa mapendekezo hayo na kujipanga kikamilifu kuyatekeleza.