Moto Mlima Kilimanjaro

0
349

Sehemu ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu zaidi Afrika unaopatikana Tanzania inawaka moto, huku juhudi za kuuzima zikiendelea.

Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA), William Mwakilema asubuhi hii amezungumza na Mwananchi na kuthibitisha kutokea kwa janga hilo.

Moto huo ulianza usiku wa jana Ijumaa Oktoba 21, 2022 na kuharibu takribani mita 4000 katika kambi ya Karanga na kuendelea hadi Mweka na sasa unakaribia Moorland ukanda wenye vichaka.

Hivi sasa zimamoto, wafanyakazi wa KINAPA, watembeza watalii na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka wanaendelea na jitihaza za kuuzima moto huo.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.