Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro imezindua zoezi la utoaji chanjo dhidi saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 14.
Katika zoezi hilo lililozinduliwa leo Aprili 23, 2024 na kutarajiwa kuhitimishwa Aprili 25, 2024, zaidi ya wasichana elfu mbili wanatarakiwa kupatiwa chanjo hiyo.
Akizungumza wakati akizindua zoezi hilo katika Shule ya Msingi Pasua, mkuu wa Wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye amesema chanjo hiyo inatolewa kwa wasichana ili kupunguza vifo vinavyotokana na saratani hiyo ya mlango wa shingo ya kizazi.