Baraza la madiwani la manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limemchagua Mhandisi Zuberi Kidumo kuwa meya wa manispaa hiyo baada ya kupata kura 27 kati ya 28 ambazo ni sawa na asilimia 96.4.
Akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Rashid Gembe amesema, kwa mujibu wa kanuni ya 4 na 10 ya kanuni za kudumu za halmashauri ya manispaa ya Moshi za mwaka 2015, Meya atashinda nafasi hiyo iwapo atapata nusu ya kura zitakazopigwa.
April 11 mwaka huu baraza la madiwani la manispaa ya Moshi lilimvua madaraka aliyekuwa meya wa manispaa hiyo Juma Rahibu kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka yake vibaya na kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kutoa vibali vya ujenzi katika maeneo mbalimbali.
Mhandisi Zuberi Kidumo ni
diwani wa kata ya Njoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).