Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na halmashauri ya Mji Geita wametiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika uandaaji wa maonesho ya kitaifa ya madini ya mkoa wa Geita, yanayotarajiwa kuanza kufanyika mwaka huu yakiwa na hadhi ya kitaifa.
Makubaliano hayo yamefikiwa na pande hizo mbili mkoani Dar es Salaam wakati wa maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba.