Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt.Elirehema Doriye, amesema mojawapo ya sifa ya mfanyabiashara kupewa kizimba kwenye soko la Biashara ni kuwa na Bima.
Dkt. Elirehema amesema kazi kuu ya Bima ni kutoa msaada pale kunapokuwa na changamoto kwa mfanyabiasha baada ya kupoteza mali kwa janga lolote linalompata.
“Tunaendelea kutoa elimu na tumekuwa tukishirikiana na TAMISEMI na Halmashauri mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu”-Amesema Dkt. Doriye.
Amesema ni ngumu kwa kampuni ya Bima kumlazimisha mtu kukata Bima kwa sababu ni suala la hiari ukiachana na Bima ya magari ambazo kisheria ni lazima ukate.