Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amefungua mkutano wa wadau wa mazingira unaojadili hali halisi,changamoto na mikakati ya kukabiliana na viumbe vamizi nchini.
Mkutano huo unafanyika mkoani Arusha ikiwa ni matokeo ya ziara ya Waziri Makamba aliyoifanya mwezi Machi mwaka 2017 katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na kubaini kuwa hifadhi hiyo inakabiliwa na tatizo la viumbe vamizi.
Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha mkoani Arusha,Wabunge, Wenyeviti na Kaimu wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali.