Mkutano wa 110 wa ILO unaendelea

0
126

Mkutano mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaendelea huko Geneva, Uswisi.

Majadiliano katika mkutano wa leo yanahusu namna nchi mbalimbali zinavyopambana na changamoto za kiuchumi.

Katika mkutano huo Tanzania inawakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako, Balozi Wa Tanzania nchini Uswisi, Maimuma Tarishi, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini ( TUCTA ) Tumaini Nyamhokia na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba-Doran.