Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amekubali barua ya kujiuzulu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar – ZAECA, ACP Ahmed Khamis Makarani.
Hatua hiyo inafuata maelekezo ya Rais Dkt. Mwinyi kuitaka ZAECA ijitathmini baada ya hivi karibuni kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG.