Mkopo wa EU kuimarisha sekta binafsi nchini

0
258

Benki ya Uwekezaji ya Ulaya imeidhinisha mkopo nafuu wa Euro milioni 540 sawa na shilingi trilioni 1.3 kwa Tanzania kwa ajili ya sekta binafsi nchini.

Mkopo huo umeidhinishwa kupitia mkataba uliosainiwa leo katika Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ukishuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Mkopo huo umetolewa kwa kuzilenga sekta ndogo na za kati zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar ambapo asilimia 30 ya fedha za mkopo huo zitatakiwa kuelekezwa kwa kampuni zinazojihusisha na masuala ya jinsia na kampuni zinazohudumu chini ya uchumi wa buluu .

Fedha hizo zilizotolewa zitawafikia walengwa kupitia benki za ndani ambazo ni CRDB, NMB na KBC.