Tanzania inatarajiwa kuwa kitovu cha maunganisho ya mawasiliano katika eneo la Afrika Mashariki na Kati kufuatia uwepo wa mkongo wa mawasiliano kituo namba mbili Afrika, pindi ujenzi wake utakapokamilika mwaka 2013.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi, alipokuwa akikagua ujenzi wa kituo na kuongeza kuwa hilo linafanyika kutokana na juhudi za serikali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha maunganisho ya mawasiliano.
Amesema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho una faida kubwa kwa Tanzania, kwa kupata mtandao wa Intaneti yenye kasi zaidi na uhakika.
“Mkongo unaokuja unapitia kusini mwa bara la Afrka, kwa hiyo tutapata uhakika wa maunganisho kwenda duniani na kusaidia sana biashara ya kuuza capacity nchini mwetu na nchi jirani, na kuwasaidia wananchi wetu na nchi jirani kuweza kushiriki katika uchumi wa kidigitali.” amesema Dkt. Yonazi