Mke wangu ni mkaguzi hodari

0
251

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema mke wake Mbonimpaye Mpango ni mkaguzi wa ndani na alikuwa mtumishi wa umma hadi pale yeye alipoteuliwa kushika wadhifa huo na kwamba kwa sasa bado anaifanya kazi hiyo nyumbani kwa uhodari.

“Mimi mwenyewe si Mkaguzi wa Ndani lakini nimekuwa karibu na Wakaguzi wa Ndani katika maisha yangu yote ya umma na maisha yangu ya kibinafsi pia, na ni kutokana na kwamba mwenza wangu ni mmoja wenu, baada ya mimi kuteuliwa nafasi ya Makamu wa Rais ikamlazimu kuacha kazi katika utumishi wa umma. Hata hivyo, ameendelea kuwa mkaguzi hodari katika kukagua nyumba yangu.” amesema Dkt.
Mpango

Mpango ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa 10 wa Shirikisho la Wakaguzi wa ndani Afrika (AFIIA).

Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali.

Arusha #TBCDigital #AFIIA