Mkataba wa ubanguaji wa zao la Korosho wasainiwa

0
186

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameshuhudia hafla ya utiaji wa saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wamiliki wa kampuni za ndani za kubangua korosho na kutoa wito kwa kampuni zingine kujitokeza na kufanya hivyo.

Waziri Hasunga amesema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuzuia usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi na kuagiza korosho zote zibanguliwe nchini.

Waziri Hasunga amesema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais John magufuli la kuzuia usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi na kuagiza korosho zote zibanguliwe nchini.

Hasunga amesema serikali imepitia vifungu vyote vya kisheria kabla ya kuanza kuingia makubaliano na kampuni hizo kwa ajili ya ubanguaji wa korosho.

Kampuni ambazo zimesaini mikataba hiyo wamesema baada ya majadiliano ya muda mrefu na serikali wameridhishwa na hatua hiyo na kwamba wataanza ubanguaji kwa wakati.

Kampuni hizo zimeingia mikataba ya kubangua korosho jumla ya Tani 7500 kwa hatua za awali huku ubanguaji huo ukitarajiwa kuanza rasmi Januari 17 mwaka huu ambapo uwezo wa kampuni hizo kubangua korosho kwa mwaka ni Tani Elfu 16 na 400