Mkandarasi mto ng’ombe atakiwa kurejea kazini

0
247

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amemtaka Mkandarasi kutoka kampuni ya CHICO anayetekeleza mradi wa ujenzi wa mto Ng’ombe wenye urefu wa kilomita 8.5 kurudi eneo la kazi na kukamilisha kazi iliyobaki.

Makalla ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kukagua mradi huo, ambapo amekuta Mkandarasi hayuko eneo la kazi licha ya kulipwa zaidi ya asilimia 60 ya fedha.

Aidha, Makalla amemuelekeza Mkandarasi huyo kuongeza nguvukazi ili kazi iweze kukamilika na kukabidhiwa kabla ya mwezi Novemba mwaka huu.

Kuhusu Wananchi waliolipwa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni sita na bado hawajaondoka, mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ameelekeza waondoke ili kumpisha mkandarasi akamilishe kazi hiyo.