Mjane wa Bilionea Msuya aachiwa huru

0
367

Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam imemwachia huru Miriam Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Bilionea Erasto Msuya na mwenzake Revocatus Everist Muyella.

Wawili hao wameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma za mauaji zilizokuwa zinawakabili

Akisoma hukumu, Jaji Edwin Kakolaki amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka haukuthibitisha tuhuma za mauaji zilizokuwa zinawakabili Miriam na Revocatus.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, Miriam pamoja na Revocatus maarufu kwa jina la Ray walikuwa wanakabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia.

Walidaiwa kumuua kwa kumchinja mdogo wa marehemu Bilionea Msuya, Aneth Msuya ambaye ni wifi yake na Miriam.

Aneth Msuya aliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali nyumbani kwake Kigamboni, Dar es Salaam, Me 25, 2016.