Mitihani ya Form VI kuanza Juni

0
281

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema mitihani hiyo itaenda sambamba na ile ya ualimu.

MITIHANI KIDATO CHA SITA KUANZA JUNI 29

Hapo jana Rais Dkt. John Magufuli ameagiza vyuo vilivyokuwa vimefungwa kutokana na janga la corona vifunguliwe Juni Mosi ambapo agizo hilo limewahusisha wanafunzi wa kidato cha sita (Form VI) wanaotarajiwa kufanya mitihani ya taifa ya kumaliza masomo yao Juni 29 hadi Julai 16 mwaka huu.