Mitandao inayoweza kutumika kiuchumi

0
139

Katika kipindi hiki cha utandawazi na matumizi ya teknolojia, mitandao ya kijamii inaweza kutumika kukuinua kiuchumi, kupata ajira ama kufanya kazi zako ziweze kujulikana na watu wengi zaidi badala ya kutumika kama mitandao ya mawasiliano pekee.

Mitandao ya kijamii inayoweza kukuza shughuli zako ni pamoja na;

LinkedIn

Mtandao huu ulioanzishwa mahsusi kwa ajili ya watu kutafuta ajira, unazidi kuwarahisishia mambo watafutaji wengi wa ajira pamoja na waajiri.

Vilevile mtandao huu unakupa uwezo wa kuchagua taarifa gani upate kulingana na aina ya kazi unayotafuta na pia kulingana na ulichosomea.

LinkedIn inakulazimu kuweka taarifa zako (CV ) na kuibadili kila wakati, huku pia ukiacha taarifa muhimu zitazomfanya mwajiri wako apate urahisi wa kukufahamu zaidi.

Lakini pia watu huweza kuweka kazi zao katika mtandao huu wa kijamii, ili kuvuta wateja kutafuta.

Ajira Portal

Huu ni ukurasa wa ajira ndani ya serikali ya Tanzania ambao pia unakuruhusu kuchagua upate taarifa wakati ajira gani zimetoka, lakini pia unaweza kuandaa taarifa zako mapema na kuzihifadhi kwenye ukurasa huu ili kurahisisha pale nafasi zinapotoka unaandaa barua pekee.

Twitter

Watu mbalimbali wamekuwa wakiutumia mtandao huu kutuma maudhui kuwa wanatafuta kazi, huku wakiomba kila anayeona ujumbe ule kuuweka kwenye akaunti yake pia ili uwafikie watu wengi.

Hivyo ujumbe huwafikia watu pwengi ndani ya kipindi kifupi.

Biashara mbalimbali zimefungua kurasa za Twitter kwa ajili ya kuonesha bidhaa kwa watumiaji wa mtandao huo.

Instagram

Kampuni, mashirika na taasisi mbalimbali kwa sasa zimefungua kurasa zao lkī katika mtandao huu wa kijamii wa Instagram, ili kufikia watu wengi zaidi na hivyo inapofika wakati wa kutangaza nafasi za kazi kurasa hizi za Instagram nazo hutumika kama njia mojawapo ya kusambaza taarifa hiyo.

Matumizi sahihi ya mitandao hii inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kumuinua mtumiaji wake kitaaluma na kiujuzi.