Mitambo ya kisasa itakayotumika MOI yawasili nchini

0
210

Baadhi ya mitambo ya kufanyia upasuaji wa ubongo bila kuvunja fuvu la kichwa cha binadamu ikiwa imewasili katika bandari ya Dar es salaam ikitokea nchini Ujerumani ilikonunuliwa na Serikali.

Mitambo hiyo itakayofungwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), imenunuliwa pamoja na vifaa vingine maalumu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.9.