Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya Dkt. Stephen Mwakajumilo amesema, uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2025 utakuwa hauna tija ikiwa miradi aliyoianzisha na kuiendeleza Rais Samia Suluhu Hassan haitasimamiwa vema.
Ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya wakati wa kusherehekea mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwakajumilo amesisitiza ushirikiano kwa chama na Serikali ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali chini ya uongozi huo wa Rais Samia Suluhu Hassan.