Taasisi ya Doris Mollel imepanga kutumia shilingi milioni 180.1 kwa ajili ya kuziwezesha hospitali za wilaya nane nchini kuwa na uwezo wa kuwahudumia watoto Njiti.
Hatua hiyo ya taasisi ya Doris Mollel inakuja zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya maadhimisho ya siku ya Mtoto Njiti Duniani Novemba 17 mwaka huu.
Katika maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani, taasisi ya Doris Mollel itakabidhi vifaa tiba ambavyo vitakwenda katika hospitali za wilaya za Serengeti, Ukerewe, Kwimba, na Magu, pamoja na ufungaji wa mitambo ya hewa ya oksijeni kwa watoto wachanga katika hospitali za Siha, Karatu na Monduli.
Taasisi hiyo itakabidhi mitungi 200 ya gesi yenye thamani ya shilingi milioji 8.2 kwa ajili ya akina mama wajawazito wilayani Serengeti.
Kutakuwa pia na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupandisha ujumbe wa watoto Njiti katika kilele cha mlima Kilimanjaro.