Mikoa 26 yapatiwa magari

0
206

Serikali imeipatia mikoa 26 ya Tanzania Bara magari, ili kuboresha utendaji kazi wa Maafisa elimu wa mikoa hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi magari hayo,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Selemani Jafo amewataka Maafisa elimu wa mikoa hiyo kuyatumia vizuri magari hayo ambayo yamegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni Mbili Nukta  Saba.

Magari yaliyokabidhiwa ni Thelathini, ambapo kati ya hayo 26 yatatumiwa na Maafisa  hao wa elimu wa mikoa  na mengine manne yatatumiwa kwa shughuli za uratibu elimu.