Miili ya watu wawili yapatikana

0
415

Miili ya watu wawili kati ya watatu waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu kwenye kata ya Moivaro eneo la Moshono jijini Arusha, imepatikana.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha,- Jonathan Shana amesema kuwa jitihada za uokoaji ili kupata mwili wa mtu mmoja uliobaki zinaendelea.

Tukio hilo limetokea majira ya saa moja asubuhi hii leo, ambapo majeruhi Wawili waliokimbia mara baada ya tukio hilo,  wanapatiwa matibabu katika hospitali  ya mkoa wa Arusha, – Mount Meru kutokana na kupata majeraha kadhaa.

Ajali hiyo ya kufukiwa na kifusi imetokea wakati watu hao Watano wakipakia Moramu hiyo kwenye Lori.