Miili ya watu watatu yapatikana

0
400

Miili ya watu wote watatu waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu kwenye kata ya Moivaro eneo la Moshono jijini Arusha, imepatikana.

Tukio hilo limetokea majira ya saa moja asubuhi hii leo, ambapo majeruhi Wawili waliokimbia kujiokoa mara baada ya tukio hilo,  wanapatiwa matibabu katika hospitali  ya mkoa wa Arusha, – Mount Meru kutokana na kupata majeraha kadhaa.

Ajali hiyo ya kufukiwa na kifusi imetokea wakati watu hao Watano wakipakia Moramu hiyo kwenye Lori.