Miili mitano yaagwa Dar

0
137

Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema,
Taifa limepoteza wataalamu muhimu katika ajali ya ndege iliyotokea mkoani Kagera tarehe 6 mwezi huu.

Dkt. Mfaume ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa shughuli ya kuaga miili ya watu watano kati ya 19 waliofariki dunia katika ajali hiyo iliyohusisha ndege mali ya Shirika la Ndege la Precision Air.

Miili hiyo ni ya watumishi wanne wa
Shirika la Afya na Maendeleo Tanzania (MDH) na mmoja kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzani (TFNC ) ambao walikuwa safarini kikazi.

Dkt. Mfaume amesema watumishi hao wote walikuwa na mchango mkubwa katika sekta ya afya na wameshiriki katika kazi nyingi za kutoa huduma za afya kwa Watanzania.

Amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwaombea marehemu hao wapumzike kwa Amani na kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni moja ya njia ya kuenzi mchango wao kwa Taifa.