Miili ya wanafamilia 14 waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea wilayani Korogwe mkoani Tanga inaagwa hii leo katika hospitali ya wilaya hiyo, Magunga.
Mara baada ya kuagwa, miili hiyo itasafirishwa kwenda Rombo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotajiwa kufanyika hapo kesho.
Katika ajali hiyo, watu 17 walifariki dunia wakiwemo wanafamilia hao 14, na wengine 12 kujeruhiwa.
Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza serikali isimamie msiba wa watu wote 17 waliofariki dunia kwenye ajali hiyo hadi utakapomalizika.