Miili 12 imepatikana hadi sasa wilayani Bunda mkoani Mara, kufuatia ajali ya kuzama kwa mitumbwi.miwili Julai 30, 2023.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani humo Augustine Magere amesema zoezi la uokoaji bado linaendelea, na kwa siku ya jana hadi kufikia saa sita usiku walikuwa wamepata miili 6.
Amesema leo alfajiri imepatikana miili minne, na hivyo kufanya idadi ya miili hiyo kufikia 12.
Magere amesema kwa sasa wanaendelea kutafuta mwili mmoja, ili kuhitimisha zoezi hilo.