Migogoro ya Ardhi Dodoma kushughulikiwa

0
254

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo @daniel_godfrey_chongolo ametaka kuwepo kwa mipango ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani Dodoma.

Chongolo ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mtekelezo, Dodoma na kuongeza kuwa lazima chanzo cha migogoro hiyo kijulikane.

Amesema haiwezekani Dodoma mahali ambapo ni Makao Makuu ya nchi kuwe na migogoro mingi ya ardhi, hivyo ni lazima wale wote ambao ni chanzo cha migogoro hiyo washughulikiwe.

Mkutano huo wa hadhara wa Katibu MKuu wa CCM ambao ni kwa ajili ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 katika majimbo yote ya mkoa wa Dodoma, umehudhuriwa na umati wa Wananchi wa mkoa huo.