Mifumo mibovu ya kupitisha maji taka ibomolewe

0
185

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila anaendelea na ziara yake ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua mkoani humo.

Akiwa na baadhi ya viongozi pamoja na watendaji kadhaa wa mkoa huo wa Dar es Salaam, Chalamika ametembelea eneo la IT Plaza, CBE, Kamata na Muhimbili ambayo yamekua yakijaa maji wakati wa mvua.

Akiwa kwenye maeneo hayo Chalamila amesisitiza suala la kuyaweka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam katika hali ya usafi.

Amesema jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji machafu kutokana na kuwepo kwa mifumo mibovu ya kupitisha maji taka ambayo amesema ni vema ikabomolewa.

“Maagizo yangu machache, jambo la kwanza tumeona watu ambao wameunganisha mifumo ya maji taka kwenye mfumo wa maji safi, Mkoa wa Dar es Salaam tangu enzi za ukoloni kuna ramani za mikondo ama mifereji ya maji. Hivyo muwatafute zaidi wale wakandarasi washiriki kuwasomea ramani za mifumo iliyokuwepo tangu mwanzo ili waweze kuwasaidia zaidi na zaidi”. Amesema Chalamila.