Miaka miwili kifo cha JPM

0
274

Watanzania leo wanakumbuka miaka miwili ya kifo cha Rais wa awamu ya Tano Dkt. John Magufuli.

Dkt. Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Alikuwa ni Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Alikuwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2021 umauti ulipomkuta.