Mheshimiwa Rais kanisa lipo pamoja nawe

0
158

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo amesema Kanisa hilo lina imani na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba litaendelea kusimama naye katika maombi na kumuunga mkono katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Dkt. Shoo ametoa kauli hiyo mkoani Arusha yanapofanyika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Amesema amelazimika kuzungumza hayo kufuatia kinaoendelea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu suala la uwekezaji wa bandari na kampuni ya DP World.

“Tuna imani na wewe Mheshimiwa Rais, tunakuamini Mheshimiwa Rais na tunaamini kwamba ukisema taasisi zako na vyombo vyako vitafanyia kazi jambo hili unamaanisha hivyo,”

“Sasa najua katika jambo hili tumeelekea mahali ambapo tunataka kugawanyika kabisa na wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na maslahi ya kiuchumi. Namshukuru Mungu amekujaalia hekima katika hili kama Mama na kiongozi umekaa kimya. Kimya chako hiki Mheshimiwa Rais sio kwamba hulifanyii kazi…..na mimi nasema jambo hili linahitaji hekima kubwa ya kuliendea na sisi kama tulivyosema tunaendelea kukuombea kwa Mungi ili hekima yote itumike katika kuweza kuleta muafaka wa jambo hili pasipo kugawanya au Wananchi kugawanyika na kutumika kama kitu cha kuchochea Wananchi kwa watu wenye maelengo yao mengine. Amesema Dkt.Shoo.