Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imemteua Mhandisi Amos Maganga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuanzia Desemba 16 mwaka huu.
REB imefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 25(1) cha Sheria namba 8 ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005.
Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Maganga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA.
Mhandisi Maganga ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya nishati, na ameshika nyadhifa mbalimbali toka alipokua ameajiriwa na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO).