Mfumuko wa bei wasalia ndani ya wigo

0
130

Serikali imesema mfumuko wa bei nchini umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa asilimia 3 hadi 5.
 
Kwa mwaka 2021 mfumuko wa bei uliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 3.7 kwa mwaka ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.3 katika kipindi cha mwaka 2020.
 
Aidha, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 3.8  mwezi Aprili mwaka  2022 ikilinganishwa na asilimia 3.3  mwezi Aprili mwaka  2021.
 
Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kulichangiwa na sababu zilizo nje ya udhibiti wa Serikali zikiwemo kuvurugika kwa mnyororo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma katika soko la dunia kutokana na athari za vita baina ya Urusi na Ukraine.
 
Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.