Meli kubwa ya watalii yatia nanga Jijini Dar es salaam

0
669

Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari nchini -TPA imeombwa kujenga kituo cha huduma za pamoja bandarini na geti maalum kwa ajili ya meli za wageni ili kuvutia meli kubwa za utalii kutumia Bandari ya DSM.

Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali wa utalii Jijini DSM wakati wa kupokea watalii waliokuja nchini na meli ya utalii ya Silver Whisper iliyotia nanga katika Bandari ya DSM.

SILVER WHISPER ni meli kubwa ya utalii,yenye uwezo wa kubeba watu 650 wakiwemo watoa huduma mbalimbali ndani yake.

Meli hii imetia nanga katika Bandari ya DSM ikiwa na watalii 333 na kati ya hao 150 watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.

Kutokana na ujio wa wageni hawa imeonekana kuwa kuna uhitaji wa kituo cha huduma za pamoja na miundombinu  rafiki ili kutoa huduma bora zaidi.