MDH NA BUDES WAHAMASISHA CHANJO KAGERA

0
157

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Bukoba Developers (BUDES) na Management Development for Health (MDH) yameunganisha nguvu ya utoaji elimu ya chanjo dhidi ya UVIKO -19 na magonjwa mengine.

Akitambulisha shirika la BUDES, Mkurugenzi wa shirika hilo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amesema, wamejikita katika sekta ya elimu, afya, mazingira, uchumi na msaada wa kisheria.

Tayari MDH na BUDES wamezindua mafunzo kwa viongozi wa mitaa na kata 14 wakiwemo wenyeviti wa serikali za mitaa, watendaji wa kata na mitaa pamoja na madiwani wa manispaa ya Bukoba ambayo yatawawezesha viongozi hao kwenda kuielimisha na kuihamasisha jamii kujitokeza na kupata chanjo dhidi ya UVIKO – 19.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema bado mwitikio wa wananchi wa mkoa huo kuiitokeza kuchanja ni mdogo, hivyo viongozi wana wajibu wa kuendelea kutoa hamasa kwa jamii ili ielewe lengo la serikali kuleta chanjo na umuhimu wake.

“Ndugu zangu serikali inayo nia ya dhati ya kuwakinga wananchi wake dhidi ya UVIKO -19, hivyo haiwezi kuleta chanjo inayodhuru watu wake.” amesema Chalamila