Uongozi wa Shirika la ndege la Precision Air umeanza mchakato wa kuwalipa fidia waathirika wote na familia zilizoathiriwa na ajali ya ndege iliyotokea tarehe 6 mwezi huu mkoani Kagera.
Hatua hiyo ya Precision imekuja zikiwa zimepita siku saba tangu kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 kuololewa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Precision Air, Patrick Mwanri amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa mchakato huo utakuwa kati ya familia za waliothirika na shirika hilo na utakuwa wa siri na utafanyika kwa umakini mkubwa.