Mbunge Martha Umbulla afariki dunia

0
227

Martha Umbulla ambaye ni Mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefariki dunia katika hospitali ya HCG iliyopo Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge Job Ndugai, Martha Umbulla amefariki dunia Januari 21 saa 7 usiku kwa saa za India.

Kufuatia msiba huo, Spika Ndugai ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza mpendwa wao.