Mbunge Kunambi aishukuru serikali

0
179

Mbunge wa Jimbo la Mlimba lililopo Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amemshukuru serikali kwa kuwezesha mchakato wa ujenzi wa barabara ya lami ya kilomita 223 kutokea Mto Rumemo Ifakara hadi Madeke ilipo boda ya Mkoa wa Morogoro na Njombe.

Kunambi amesema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara katika Kata za Masagati na Utengule ambapo ameeleza kuwa kwa kuanzia tayari maelekezo yameshaanza ya kuanza kwa awamu ya kwanza ya ujenzi huo ambapo utaanza na kilomita 50 kuanzia Ifakara hadi Mbingu kisha awamu ya pili yenye kilomita 37 kuanzia Mbingu hadi Chita itafuata.

“Kama hiyo haitoshi kupitia mahusiano mazuri aliyoyaweka Rais Samia tumepata ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambapo wao watawezesha ujenzi wa kilomita 93 kwa kiwango cha lami kutokea Kihansi Mlimba hadi Madeke Njombe, hapa uchumi wa wananchi wa Mlimba utakua umefunguka kwa kiwango kikubwa,”Amesema Kunambi.