Mbunge akabidhi vifaa vya ujenzi

0
261

Mbunge wa jimbo la Mbogwe mkoani Geita, – Nicodemus Maganga amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi cha Ilolangulu, ujenzi wa zahanati katika kata ya Bukandwe pamoja na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi iliyopo katika kata hiyo ya Bukandwe.

Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na mifuko 100 ya saruji na bati elfu moja, vimekabidhiwa kwa Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, – Pendaeli Mazengo.

Kuhusu ujenzi wa kituo cha polisi cha Ilolangulu, Maganga amesema ametoa vifaa hivyo vya ujenzi ili kituo hicho kikamilike, na hivyo kusaidia kupunguza vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara katika eneo hilo.