Mbowe, Matiko wateta na Wanahabari

0
524

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amewaomba Jaji Mkuu wa Tanzania, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Kamishna Jenerali wa Magereza kufanya operesheni safisha magereza ili kupunguza idadi kubwa ya mahabusu ambao hawapaswi kukaa mahabusu.

Mbowe ametoa ombi hilo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari na kufafanua kuwa gereza la Segerea  lililopo mkoani Dar es salaam lina uwezo wa kukaliwa na mahabusu 750 lakini kwa sasa kuna zadi ya mahabusu Elfu Mbili.


Kuhusu suala la Joshua Nasari kuvuliwa ubunge wa Arumeru Mashariki kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, Mbowe amemtaka Nasari kuzungumzia jambo hilo hii leo.


Kwa upande wake Mbunge wa Tarime Mjini mkoani Mara, -Esther Matiko ameiomba serikali kuwapeleka hospitali mahabusu wenye matatizo ya akili na sio kuachwa mahabusu bila kupatiwa msaada.

Mapema mwezi huu, Mbowe na Matiko waliachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam baada ya kukaa gerezani kwa takribani miezi mitatu kwa yuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali.