Mbowe : Lowassa alikuwa Mwanasiasa mahiri

0
327

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ametuma salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wapenda demokrasia wote kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mbowe amesema Lowassa alikuwa kiongozi shupavu, mwanasiasa
mahiri, mwanaharakati hodari na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini.

“Alikuwa rafiki yangu na mshirika katika safari ya kuleta demokrasia ya kweli Tanzania. Alikuwa mtu mwenye hekima, busara, ujasiri, uzalendo, mtu mwenye huruma, upendo na msamaha kwa wote. Alikuwa mtu mwenye maono, mipango na mtekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya Wananchi,” Amesema Mbowe.

“Nimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo
chake. Nimepoteza rafiki, ndugu na mshauri mzuri. Tanzania na Dunia imepoteza kiongozi shujaa, mwenye mchango mkubwa katika kujenga amani, ushirikiano na ustawi wa jamii,” Amesema