Mbolea ya ruzuku ilindwe

0
157

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuwa walinzi wa mbolea ya ruzuku iliyotolewa na serikali, ili kuhakikisha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Amesema kuna baadhi ya watu si waalinifu ambao wamekuwa wakitorosha mbolea kwenda nchi jirani na kuwaacha watanzania bila kuwa na mbolea ya kutosha.

”jambo hili lazima tulikemee na tulisimamie sote ili kuhakikisha mbolea iliyopo nchini ni kwa ajili ya watanzania, kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzake.” amesisitiza Waziri Mkuu

Ametoa kauli hiyo wakati akisalimia na wananchi kwenye eneo la Mbalizi mkoani Mbeya, akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani humo.

Ameongeza kuwa utoaji wa ruzuku hiyo ya mbolea unalenga kuongeza uzalishaji wa chakula nchini na ni marufuku kuiuza nje ya nchi.