Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe imekamata marobota ya mbolea ya ruzuku ambayo ni bandia, iliyokuwa imefichwa katika nyumba moja ambayo kwa sasa haikaliwi na mtu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka amesema, wafanyabiashara watakaobainika kuhusika na biashara hiyo watafiilisiwa.
Amesema mmiliki wa mbolea hiyo ya ruzuku ambayo ni bandia kwa sasa anachunguzwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pamoja na kukamatwa kwa mbolea hiyo bandia, kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Njombe pia imekamata viroba vilivyochapishwa majina ya aina mbalimbali ya mbolea, mashine za kushonea viroba pamoja na nyuzi za kushonea.