Mbatia azungumzia corona, aipongeza Serikali

0
227

Chama cha NCCR Mageuzi kimeipongeza Serikali kwa kulitambua janga la corona, na kuchukua hatua za kuhamasisha Wananchi kujinga na janga hilo.
 
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa James Mbatia, Wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam.

Ameshauri kufanyika kwa tathmini ya corona nchini, itakayosaidia kuwekwa vipaumbele na usimamizi utakaosaidia  kukabiliana na maambukizi zaidi.
 
Aidha, Mbatia amesema kuwa takwimu za  ugonjwa wa corona Barani Afrika zinaonesha katika wimbi la tatu la ugonjwa huo kuna ongezeko la asilimia 43 ya maambukizi ikilinganishwa na wimbi la kwanza na la pili, hivyo tahadhari zaidi inahitajika.