Mbarawa : Barabara ya Tabora-Koga-Mpanda kukuza utalii

0
238

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda kutasaidia kukuza utalii wa mikoa ya Tabora na Katavi kutokana na kuwepo kwa usafiri wa uhakika kwa watalii watakaokwenda kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mikoa hiyo.

Profesa Mbarawa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda yenye urefu wa kilomita 342.9 ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 473.9.

Profesa Mbarawa amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara hiyo kuitunza ili idumu kwa muda mrefu.

Ameeleza kusikitishwa na wizi wa nguzo za taa zilizowekwa katika barabara hiyo na kuwataka Wananchi kuripoti vitendo hivyo vya wizi kwenye mamlaka husika.