Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye mazungumzo ya hapa na pale ndani ya ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, ambapo hii leo mkutano wa nane wa Bunge la 12 unafikia tamati.
Mbali na kipindi cha maswali na majibu, serikali itawasilisha muswada wa sheria ya Bima ya afya kwa wote ambao utasomwa kwa mara ya kwanza.
Hii leo pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atatoa hoja ya kuahirisha Bunge.